Kitengo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UCC) kinapenda kuwatangazia majina ya waliochaguliwa kwenye nafasi ya kazi ya muda mfupi kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama maonyesho ya Sabasaba, kwamba wanatakiwa kufika siku ya Jumatatu 19/6/2017 saa 2 kamili asubuhi kwenye jengo la UCC Makao makuu kwa ajili ya kuchukua barua zao za wadhamini. Barua hizo zitaanza kutolewa kuanzia saa 2 kamili asubuhi hadi saa 3 kamili asubuhi siku hiyo ya Jumatatu 19/6/2017.