Kitengo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UCC) kinawataarifu wale wote waliopendekezwa kwenye usaili wa kazi ya muda mfupi kwenye maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama maonyesho ya Sabasaba, kwamba wanatakiwa kuja siku ya Jumamosi tarehe 17/6/2017 saa 2 kamili asubuhi kwenye jengo la UCC makao makuu kwa ajili ya usaili. Wote waliopendekezwa waje na vyeti halisi.