
Rejea Tangazo la Kazi ya muda mfupi lililotolewa Julai 22, 2023 katika tovuti (www.ucc.co.tz) ya Kitengo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UCC) kwa ajili ya kutoa huduma ya uendeshaji wa Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane kwa mwaka 2023 yatakayofanyika Mkoani Mbeya. Maonesho haya yatakayoanza Agosti 1 hadi Agosti 8, 2023 kwenye viwanja vya John Mwakangale vilivyopo Mkoani Mbeya.
UCC inapenda kukutaarifu kuwa kutokana na vigezo vilivyoweka katika tangazo letu waombaji wote 145 walioomba wamekidhi vigezo vilivyowekwa kwa waombaji. Hivyo, waombaji wote 145 wamechaguliwa kuingia katika usaili wa hatua ya kwanza (Aptitude test).
Waombaji ambao majina yao yameorodheshwa wanatakiwa kujiandaa kwaajili ya usaili huo wa hatua ya kwanza. Usaili huo utafanyika kwa njia ya mtandao (Online Test) kupitia tovuti https://lms.ucc.co.tz/ siku ya tarehe Julai 27, 2023. Usaili utakuwa ni wa muda wa dakika Arobaini (40) tu. Ratiba na orodha ya majina bonyeza hapa TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI AWAMU YA KWANZA.