University of Dar es salaam Computing Centre

Excellence, Innovation and Technological Foresight

KUFUNGULIWA KWA CHUO TAREHE- 01 -06- 2020

Ndugu Wanafunzi,

Kitengo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UCC) kinapenda kuwaatarifu wanafunzi wake wote kuwa kufuatia maelekezo ya serikali kuhusu kufunguliwa kwa vyuo vikuu nchini, mnaombwa kuzingatia yafuatayo:-

 

1. Wanafunzi wanaondelea wanahitajika kufanya usajili ikiwa ni pamoja na ulipaji wa ada na kwa wale wapya watahitajika kufika chuoni ili waweze kufanyiwa usahili. Utaratibu wa kulipa ada unafanyika kwa kutumia kumbukumbu namba (Control Number) ambayo inapatikana kwenye tovuti ya http://aris.ucc.co.tz

 

2. Kufika chuoni tarehe 1/6/2020 ili kuanza masomo rasmi.

 

3. Kufuata  taratibu zote kama zinavyoelekezwa na Wizara ya Afya kuhusu kujikinga na COVID-19 ikiwa ni pamoja na uvaaji wa Barakoa (Mask).

 

Kwa mawasiliano zaidi unawezaz wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo;

1. 0713 348 731 - Makao Makuu

2. 0735 592 848 - City Centre

3. 0762 533 393 - Dodoma 

4. 0783 566 863 - City Centre

5. 0713 570 024 - Makao Makuu