University of Dar es salaam Computing Centre

Excellence, Innovation and Technological Foresight

MAREKEBISHO YA MUDA WA USAILI-TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI YA MUDA MFUPI SABASABA 2020

Rejea Tangazo la Kazi ya muda mfupi lililotolewa Juni 16, 2020 katika tovuti (www.ucc.co.tz) ya Kitengo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UCC) kwa ajili ya kutoa huduma katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama Maonesho ya Sabasaba yatakayoanza Julai 01 hadi Julai 13, 2020 kwenye viwanja vya Maonesho vya Sabasaba vilivyopo barabara ya Kilwa, Temeke - Dar es Salaam.

UCC inapenda kukutaarifu kuwa kutokana na vigezo vilivyoweka katika tangazo letu waombaji 541 kati ya 737 wamekidhi vigezo vilivyowekwa kwa waombaji. Hivyo, waombaji 541 wamechaguliwa kuingia katika usaili wa hatua ya kwanza (Aptitude test).

Soma kiambatanisho hapa kwa maelezo zaidi